September 24, 2016

Chelsea kusafiri hadi ugani Emirates kuchuana na Arsenal

Meneja Antonio Conte anasema anahitaji mda kuimarisha timu yake Chelsea kucheza anavyotaka yeye ili ipate matokeo bora.
Chelsea walitoka sare na Swansea, wakapoteza mechi yao dhidi ya Liverpool kabla ya kuchapa Leicester City 4-2 kwenye mechi zao za hivi majuzi.
Chelsea wanakutana na Arsenal Jumamosi huku meneja Arsene Wenger akiwa anatafuta ushindi wa kusherehekea vizuri miaka 20, ifikapo 1 October, tangu achukue usukuani wa the Gunners.
Kibarua cha Conte hata hivyo si rahisi- Msimu wa ligi uliopita Chelsea walibugia magoli 53.
Katika mechi ya jumamosi Arsenal watajaribu kumaliza matokeo mabaya dhidi ya the blues za hivi maajuzi uku pia wakizingatia nidhamu ya hali ya juu kuepuka kupewa kadi nyekundu kama mechi zilizopita.

September 22, 2016

NTSA itatupilia mbali leseni za magari yanayokiuka sheria za trafiki

Mamlaka ya uchukuzi na usalama bara barani NTSA limesema linapanga mkakati wa kufuta leseni za magari yote yanayopatikana kutotimiza matakwa ya sheria za trafiki. 

Msimamizi mkuu wa NTSA  Samwel Msumba anasema magari yatakayolengwa ni yasiyokuwa na vidhibiti mwendo. Akizungumza katika kituo cha kibiashara cha Salgaaamesema madeeva wengi wameendelea kuvingoa vidhibiti mwendo kinyume cha sheria.

Rais wa Botswana amtaka rais Mugabe kujiuzulu

Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu mara moja na kuruhusu mtu mwingine kuchukuwa uongozi wa taifa hilo linalokabiliwa na msukosuko wa uchumi na kisiasa. 

Khama amedai Mugabe hana tena uwezo wa kuinua uchumi wa nchi yake, na umri wake haumruhusu kukabiliana na hali hiyo.

Maafisa zaidi watumwa kuimarisha usalama Garissa

Maafisa zaidi wametumwa kuimarisha usalama kaunti ya Garissa badaa ya waasi wa Al shabab kuvamia kituo cha polisi cha Hamey mapema leo na kutekeleza uharibifu.

 Inadaiwa wasi hao wamefanikiwa kuwajeruhi maafisa 2 huku wengine 4 wakiwa hawajulikani waliolo. Wamefanikiwa pia kutoweka na silaha,magwanda ya polisi pamoja na gari moja.

JSC kumtaja jaji mkuu mpya kesho

Tume ya huduma za mahakama ikisubiriwa kumtaja jaji mkuu mpya kufikia kesho, Wasomi wa sheria nao wanamapendekezo yao kando. Kuna wale wanaompigia upatu jaji wa mahakama ya juu Smokin Wanjala wenguine nao jaji David Maraga.

ODM yakashifu viongozi wanaopinga uteuzi wa Laban Ayiro kama kaimu chansela wa chuo kikuu cha Moi

Chama cha ODM kimewalaani viongozi wa kisiasa wanaopinga uteuzi wa prof Laban Ayiko kama kaimu naibu chansala wa chuo kikuu cha Moi. Kinasema hatua hiyo ni ishara kwamba viongozi wa sasa wamegubikwa na ukabila. 

Mbunge wa busia Florence Mutua ameitaka tume ya haki na maridhiano NCIC kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi hao na kuongeza hakuna nafasi ya ukabila humu nchini

Gavana Kidero akubali kumlipa Ondiek milioni 8.8 kwa kumuondoa afisini bila kuzingatia sheria

Gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero amekubali kumlipa milioni 8.8 aliyekuwa waziri wa mazingira katika bunge la Nairobi Evans Ondiek kwa kumuondoa afisini bila kuzingatia sheria. Katika waraka, 

Kidero ameridhia agizo lililotolewa na mahakama agosti 22. Ondiek aliwasilisha kesi mahakama akidai Kidero alimfurusha uongozi kwa sababu za kisiasa, madai ambayo Kidero alipinga akidai hatua yake ilinuia kuhakikisha utendakazi bora katika kaunti.

Jaji David Maraga ateuliwa kuwa jaji mkuu wa Kenya

Jaji David Maraga ameteuliwa kuwa jaji mkuu wa Kenya.Ni uteuzi uliofanywa na tume ya huduma za mahakama baada ya kuwahoji watu 14 waliokuwa 

wametuma maombi ya kujaza nafasi hiyo.Jina la Maraga sasa litawasilishwa kwa rais Uhuru Kenyatta kwa uteuzi rasmi.Mwenyekiti wa LSK Tom Ojienda ametetea uamuzi wa JSC kumteua Maraga.